Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 21Article 558727

Habari za michezo of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Molinga, Chirwa Waamsha Dude Namungo

Molinga, Chirwa Waamsha Dude Namungo Molinga, Chirwa Waamsha Dude Namungo

KOCHA mkuu wa Namungo, Hemed Morocco amesema ujio wa washambuliaji David Molinga na Obrey Chirwa ndani ya timu hiyo utaifanya kuwa tishio ndani ya msimu ujao wa ligi kuu.

Chirwa na Molinga wote kwa pamoja wamewahi kuwa wachezaji wa Yanga katika misimu tofauti ikiwa ndiyo mara yao ya kwanza kucheza ndani ya ligi kuu ambapo timu hiyo ndio iliyowaleta nchini kucheza soka la Tanzania kwa mara ya kwanza japo kwa sasa wote wametua Namungo.

Akizungumza na Championi, Morocco alisema kuwa kuongezeka kwa wachezaji hao wazoefu ndani ya klabu hiyo kuitaiongezea makali katika safu ya ushambuliaji jambo ambalo anaamini litaipa makali Namungo na kuwa klabu ya kuogopwa katika msimu ujao wa ligi kuu.

“Molinga na Chirwa ni wachezaji wazoefu wa ligi ya Tanzania lakini ni wachezaji wazuri katika eneo lao la ushambuliaji, hakuna ambaye hafahamu ubora wa wachezaji hawa na mambo ambayo wameyafanya katika ligi kuu.

“Hivyo kuingia kwao ndani ya Namungo msimu huu kuitaiboresha safu yetu ya ushambuliaji ambapo tunaamini mchango wao utakuwa mkubwa na utafanya timu nyingi kuihofia Namungo kuelekea msimu ujao,”alisema kocha huyo.