Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 27Article 554074

Soccer News of Friday, 27 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Morisson Mwalimu wa Kiswahili Simba SC

Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison

Kumbe yule mzee wa kuwakera, fundi wa Soka kutoka Ghana kiungo Benard Morisson, ukiachana na soka bado ni mzungumzaji mzuri wa Kiswahili na anajitoa kufundisha na wenzake ndani ya Klabu hiyo.

Winga mpya wa Simba, Peter Banda amesema kuwa ameanza kuyazoea mazingira mapya ya klabu hiyo kupitia kwa Bernard Morrison ambaye mara nyingi amekuwa akimchangamsha na kumfundisha namna ya kuzungumza Kiswahili kwa haraka zaidi.

Banda amesajiliwa na Simba katika dirisha hili kubwa la usajili akitokea katika Klabu ya Nyassa Big Bullet ya nchini Malawi ambapo winga huyo anatabiriwa kuja kurithi mikoba ya Luis Miquissone aliyetimka ndani ya klabu hiyo.

“Morrison mara nyingi amekuwa akinitania kupitia wachezaji wa Simba, ghafla nimejikuta nikitaniana na wachezaji wengi jambo ambalo limenifanya niwazoee mapema wachezaji wengi wa Simba, sipo kimya kama mara ya kwanza wakati tunaanza safari ya kuelekea Morroco kwa sasa nimechangamka zaidi.

“Morrison pia amekuwa akinihimiza kujifunza jinsi ya kuongea Kiswahili kwa haraka, mara nyingi huwa ananifundisha maneno machache ya Kiswahili na mara nyingi nikikosea huwa anafurahi akinihimiza nisikosee, namshukuru sana,” amesema winga huyo.