Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 12Article 562672

Soccer News of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Morisson ni mpango kazi wa Gomes

Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison

Licha ya matukio yake ya kila siku kumbe kocha mkuu wa Simba SC Didier Gomes anauelewa na kuutambua vyema uwezo wa Morisson akiwa uwanjani.

Hiyo ni kutokana na Kocha kuyo kummwagia sifa kadhaa akisifia ubora wa mshambuliaji huyo asiekauka kwa vituko katika midomo ya wapenda soka.

Katika kuthibitisha hilo Gomes amekwenda mbali na kusema iwapo mchezaji huyo anakueppo uwanjani basi madhara yake ni makubwa kwa wapinzani kama hatafunga goli lazima atatoa usaidizi wa goli.

Morisson anajiandaa kuwakabili Jwaneng Galaxy ya Botswana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Kwa upande wa michezo ya ligi hatimae amemaliza adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu.