Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 14Article 542623

Habari za michezo of Monday, 14 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Morocco apigia hesabu pointi 12 Namungo FC

Morocco apigia hesabu pointi 12 Namungo FC Morocco apigia hesabu pointi 12 Namungo FC

Kauli hiyo ya Morocco inakuja kutokana na baadhi ya makocha wa timu za Ligi Kuu kukabidhi ripoti zao mapema kwa uongozi kwa ajili ya mapendekezo ya usajili wa msimu mpya.

Akizungumza na gazeti hili jana, Morocco alisema kutokana na mechi ngumu zilizopo mbele yao na kuhitaji kupata pointi ili kumaliza katika nafasi nzuri kwenye ligi hiyo, kunamfanya achelewe kukabidhi ripoti hiyo, hivyo kusubiri hadi mwishoni mwa msimu.

Alisema kwa sasa kikosi chake kipo Musoma tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Biashara United utakaopigwa kesho, Jumanne.

"Tumeshafika Musoma kwa ajili ya mechi yetu dhidi ya Biashara United, ni mechi ngumu na ya ushindani mkubwa, ila tumejipanga kuhakikisha tunafikia malengo yetu ya kumaliza tukiwa katika nafasi ya nne za juu katika msimamo.

"Kwa sasa nina pointi 41, ili nimalize nafasi nne za juu lazima nishinde mechi zote hizo, tunahitaji kupambana hali ambayo akili na nguvu kuelekeza katika malengo hayo, suala la usajili litakuwapo baada ya kumaliza msimu," alisema Morocco.

Alisema wanapambana kutafuta  pointi tatu katika mchezo huo baada ya hapo watarejea jijini kucheza dhidi ya Azam FC, Ruvu Shooting pamoja na Simba mechi ambazo zote ni ngumu kwao.

Namungo iko nafasi ya nane ikiwa na pointi 41 na imebakiza mechi dhidi ya Biashara United, Azam FC, Ruvu Shooting na Simba, na endapo ikishinda zote itakuwa imekusanya pointi 53.