Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 584800

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Morocco yaichapa Ghana 1-0 Kundi C

Morocco wameanza vyema kampeni ya kuwania ubingwa wa AFCON Morocco wameanza vyema kampeni ya kuwania ubingwa wa AFCON

Morocco wameanza vyema kampeni ya kuwania ubingwa wa Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON 2021 baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Ghana mtanange wa kwanza Kundi C.

Bao pekee kwenye mechi hiyo limefungwa na Sofiane Boufal ambaye anakipiga kunako klabu ya Southamption kunako dakika ya 82 ambapo bao hilo linakuwa la kwanza katika mechi 23 za Morocco.

Baada ya goli hilo, Ghana waliamka na kuonyesha kandanda safi lakini muda ulikuwa umeisha kuweza kupata goli. Ushindi huo bila shaka utakuwa mzuri kwa taifa la Afrika Kusini ambalo lilikuwa linadhani wao ndiyo wanastahili kushiriki.