Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 585937

African Cup of Nations of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Morocco yapeta AFCON

Morocco yaichapa Comoro 2-0 Morocco yaichapa Comoro 2-0

TIMU ya taifa ya Morocco imeendeleza wimbi la ushindi katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuichapa Comoro mabao 2-0 usiku wa Ijumaa katika mchezo wa Kundi C Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé.

Mabao ya Morocco yamefungwa na kiungo wa Standard Liège ya Ubelgiji, Selim Amallah dakika ya 16 na mshambuliaji wa Alkmaar Zaanstreek ya Uholanzi, Zakaria Aboukhlal dakika ya 89 na kwa ushindi huo, Simba wa Atlasi wanafikisha pointi sita na kufuzu Hatua ya mtoano ya michuano hiyo mbele ya Gabon yenye pointi nne, Ghana moja na Comoro ambayo haina pointi.

Mechi nyingine ya Kundi C jana, Gabon ilitoa sare ya 1 -1 na Ghana hapo hapo Ahmadou Ahidjo, Yaoundé.

Ghana ilitangulia kwa bao la mshambuliaji wa Al Sadd ya Qatar, André Ayew dakika ya 18, kabla ya mshambuliaji wa Marmande ya Ufaransa, Jim Émilien Ngowet Allevinah kuisawazishia Gabon dakika ya 88.