Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 05Article 541198

xxxxxxxxxxx of Saturday, 5 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Morrison: Nini...Thubutuu!

STAA anayewakosha zaidi mashabiki wa Simba kwa sasa, Bernard Morrison ametamka kwamba kwa sasa hathubutu wala haoni haja ya kujibizana na Yanga.

Morrison ambaye ni raia wa Ghana mwenye uzoefu na soka na ameenda mbali zaidi kwa kusisitiza kwamba; “nakaa kimya, kazi itaongea.”

Morrison alisajiliwa na Yanga mwaka 2019 ambapo aliichezea msimu mmoja kabla ya msimu huu kusajiliwa na Simba, lakini akazua utata mkubwa baada ya Yanga kupeleka malalamiko TFF wakidai bado mchezaji huyo ana mkataba na klabu hiyo.

Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji chini ya aliyekuwa mwenyekiti Elias Mwanjala.

Kamati hiyo ilitoa hukumu kwamba Morrison ni mchezaji huru ikidai mkataba wake na Yanga ulikuwa na upungufu.

Uamuzi huo uliwakera Yanga na kuamua kukata rufaa na kupeleka suala hilo katika Mahakama ya usuluhishi ya michezo (CAS) na sasa wanadai wanasubiri kusikilizwa na kutolewa uamuzi kwa kesi hiyo.

Mwanaspoti ambalo ndilo gazeti pekee la Kiswahili linalochapishwa Tanzania na Kenya, lilimtafuta Morrison ambaye alijibu kwa kifupi kwamba hata wakala wake amemuonya kuzungumzia ishu hiyo.

“Sitamani kuongea lolote, wakala wangu amenikataza na kunitaka nifanye kazi basi,” alisema Morrison na kuongeza kuwa mengine ambayo yanaendelea anayaacha kama yalivyo.

Morrison aliyesaini mkataba wa miaka miwili amekuwa mchezaji nyota katika kikosi cha Simba kutokana na mchango mkubwa anaoutoa ndani ya timu hiyo kwasasa.

Katika kikosi cha Simba Morrison amekuwa akifunga mabao muhimu na hadi sasa ametupia nyavuni mabao manne pamoja na kutoa pasi za mwisho nyingi ambazo wachezaji wenzake wamezitumia kufunga.

Mchezaji huyo amekuwa hatari dhidi ya timu pinzani haswa Simba wanapokuwa wanashambulia.

Join our Newsletter