Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 24Article 553447

Soccer News of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Msimu ujao nataka nifanye maajabu" - Makapu

Saidi Juma Makapu Saidi Juma Makapu

Beki Juma Makapu aliesajiliwa na Polisi Tanzania, amesema msimu ujao anautazama kama ukurasa mpya katika maisha yake ya soka hivyo anataka kuandika rekodi nzuri pekee kwa kuwa atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Makapu amejiunga na Polisi Tanzania baada ya kuachwa na Yanga ambayo aliitumikia kwa muda wa miaka saba, amesema ana madini mengi mguuni kwake yatakayoipa faida timu yake ya sasa kwa kuwa uzoefu nao unakwenda kumsaidia.

"Yanga ni kama chuo cha soka kwangu, nimejifunza mengi katika miaka saba hiyo,nitaanza kuyafanyia kazi msimu unaokuja," amesema Makapu na ameongeza kuwa;

"Wengi wanaweza wakajiuliza nilishindwaje kucheza Yanga, ipo hivi Yanga ni timu yenye ushindani mkubwa sana, tofauti na timu yangu mpya ambapo ninaamini nitapambana na kocha atafurahia kiwango changu,"amesema.

Polisi Tanzania inafanya Jitihada kubwa chini ya Mwalimu Malale Hamsini kuhakikisha wanajenga kikosi chao kwa ajili ya Mapambano ya Msimu ujao.