Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 27Article 554038

Soccer News of Friday, 27 August 2021

Chanzo: eatv.tv

''Msizikimbilie haraka Yanga na Simba'' Juma Abdul

Mchezaji wa zamani wa Yanga, Juma Abdul Mchezaji wa zamani wa Yanga, Juma Abdul

Beki wa zamani wa Taifa Stars, Juma Abdul ametoa angalizo kwa Wachezaji wanaohitajika na klabu za Simba na Yanga kufanya maamuzi kwa weledi mkubwa kabla ya kujiungana wakongwe hao wa soka hapa nchini ili kuepusha kuharibu vipaji vyao.

Juma Abdul ambaye aliichezea Yanga kwa mafanikio, amesema ni vyema wachezaji wanaochipukia kuhakikisha wanapoamua kujiunga na vilabu hivyo wahakikishe wanauwezo wa kupigania nafasi ya kucheza.

''Nadhani ni vyema wachezaji wanaohitaji kujiunga na Simba hata Yanga wanapaswa kupigania nafasi ya kucheza mara kwa mara, kivyume na hapo wataishia kutolewa kwa mkopo na biashara yao itaishia hapo'' amesema Juma Abdul.

Beki huyo wa kulia ambaye aliwahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa TPL, kwasasa amejiunga na DTB inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza(Championship) msimu wa 2021/2022.