Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 28Article 544504

Habari za michezo of Monday, 28 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Msolla awarudisha waliosimamishwa

Msolla awarudisha waliosimamishwa Msolla awarudisha waliosimamishwa

Uongozi wa Yanga umetangaza kuwarudisha kundini wajumbe wao watatu waliosimamishwa na klabu hiyo.

Akitangaza uamuzi huo Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla amesema kikao cha kamati ya utendaji kimetoa uamuzi huo.

Msolla amesema Rogers Gumbo, Frank Kamugisha na Salim Rupia sasa wanarejea katika nafasi zao za wajumbe wa kamati ya utendaji na kuendelea na majukumu yao.

"Tumekubaliana tuwarudishe tuendelee na umoja na sasa naomba kama wapo hapa waje huku mbele katika nafasi zao," amesema Msolla.

"Lengo la maamuzi haya ni kutaka kurudisha umoja wa klabu yetu na tuendelee na umoja wa klabu yetu kama kawaida yetu."

Hata hivyo wakati wajumbe hao wakiitwa kila mmoja ni Gumbo pekee aliyekuwa ndani ya ukumbi huo.

Related Manji atua, apagawisha wanachama mkutano YangaKikwete ndani mkutano wa Yanga


JK, Manji wafunika mkutano mkuu Yanga


Katibu mkuu TFF akumbana na zomeazomea mkutano Yanga"Hawa ambao hawapo nitamuagiza katibu mkuu awaandikie taarifa rasmi ya maamuzi hayo."

Wajumbe hao watatu walisimamishwa na Yanga wakidaiwa kupinga mambo mbalimbali ya klabu hiyo.