Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 09Article 541915

Habari za michezo ya

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Msuva Atajwa na Mabosi wa Yanga

Msuva Atajwa na Mabosi wa Yanga Msuva Atajwa na Mabosi wa Yanga

Msuva Atajwa na Mabosi wa Yanga June 9, 2021 by Global PublishersMABOSI wa Yanga wanahaha kumpata winga matata wa aina ya Simon Msuva anayekipiga hivi sasa Klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco.

Msuva aliichezea kwa mafanikio Yanga kabla ya kutimkia Difaa El Jadida ya Morocco kabla ya kuuzwa msimu huu Casablanca anayoichezea hivi sasa.

Msuva tangu ameondoka Yanga, timu hiyo imekosa winga wa aina hiyo mwenye uwezo wa kufunga na kutengeneza mabao kwa wenzake.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, katika kukiboresha kikosi chao, Yanga imepanga kumsajili winga mwenye kasi anayefanana na Msuva.Mtoa taarifa huyo alisema kuwa tangu ameondoka Msuva, Yanga imekosa mbadala wake mzuri mwenye uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi za kufunga.

“Ukweli upo wazi kabisa, tangu Msuva ameondoka Yanga tumekosa mbadala wake mwenye sifa za kufunga na kutengeneza nafasi kwa wachezaji wenzake.

“Msuva alikuwa na sifa zote za winga ya kwanza kasi, kufunga na kutengenea mabao kwa kupitia pembeni akipiga krosi safi kwa wachezaji wenzake.“

Katika mipango ya usajili katika msimu huu, uongozi umepanga kumsajili winga na nafasi nyingine lakini hiyo itakuwa mojawapo,” alisema mtoa taarifa huyo.

Yanga kwa kupitia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano, Injinia Hersi Said, juzi alisema: “Tumepanga kufanya usajili bora na kisasa utakaoendana na hadhi ya timu yetu, jukumu hilo lote la usajili tumeliacha kwa benchi la ufundi.”

Stori: WILBERT MOLANDI, Dar

Join our Newsletter