Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 18Article 552184

Soccer News of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Mtibwa, Kagera zimeacha kushindana na vigogo

Aliyewahi kuwa kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila Aliyewahi kuwa kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila

Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema kuwa wakatamiwa hao wameporomoka kiwango tofauti na miaka kadhaa iliyopita na hii ni kwakuwa wameacha kushindana na vilabu vya Simba na Yanga.

Katwila ambaye alikuwepo kwenye kikosi cha mafanikio cha Mtibwa Sugar kilichotwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania bara mara mbili mfululizo miaka ya 1999 na 2000, amesema kumekuwa na mabadiliko ya uendeshaji wa timu ambao anaamini ndio kumepelekea kuzorota kwa timu hiyo.

''Mtibwa ya zamani ina utofauti mkubwa sana na ya zamani kuanzia kwenye usimamizi wake wa viongozi ,huduma kwa wachezaji ''

''Mtibwa ilikuwa ina uwezo wa kumsajili mchezaji ambaye alikuwa anawaniwa na Simba na Yanga, kadri muda ulivyokuwa unaenda ikasalia kuwa timu ya kuzalisha vipaji na baadae kuwauza baadae kwa wakongwe hao wa mpira nchini.

''Ukiacha kushindana na vilabu vya Simba na Yanga basi wewe unabaki kuwa kama mshiriki''

''Mtibwa Sugar na Kagera Sugar siwezi kusema inazalisha wachezaji, kipindi kile makocha walifanya kazi kubwa kutengeneza vipaji, hata Simba na Yanga zilikuwa zinatupia macho kwenye hizi timu kusajili wachezaji wazawa hivyo tulikuwa tunawauza na timu ikawa inapata pesa, kwakuwa mpira ni biashara pia''

''Mameneja wengi wa hivi karibuni waliokuwa wanaingia kwenye hivi viwanja, wengine wanakuwa hawapendi mpira kwakuwa hawaoni hela yoyote inayoingia kupitia klabu, matokeo yake ataanza kwenda tofauti na timu, huwezi ukawa unagharamia kusajili wachezaji tu halafu usione kinachorejea, '' amesema Katwila

Kocha huyo kwa sasa anaifundisha Ihefu ya Mkoani Mbeya , amewaasa viongozi wa timu hiyo kuwa kitu kimoja ili kurejesha ushindani uliokuwepo kwa miaka mingi iliyopita.