Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 29Article 560323

Soccer News of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

"Mugalu Anaichelewesha Simba"- Oscar Oscar

Mshambuliaji Chriss Mugalu Mshambuliaji Chriss Mugalu

Mchambuzi maarufu wa soka nchini, Oscar Oscar amesema; “Chris Mugalu ni kama anaichelewesha Simba SC ni aina ya mchezaji anaehitaji nafasi kama tano kupata goli moja.

Anaweza akawa na sifa nyingine zote ila shida yake ndio hiyo, Simba inachelewa kwenye mechi nyingi sana kwa kumtegemea Mugalu,” amesema Oscar Oscar wakati akijibu swali la Fatma Likwata aliyetaka kujua kama ni wakati sasa wa kuendelea kumuamini Kagere kwa kuwa Mugalu anaoesha Ku-Struggle.

Mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga, Mugalu alipata nafasi nyingi za wazi lakini hakuweza kuzitumia vizuri kupata matokeo na mwisho wa siku Yanga wakaibuka na ushindi wa bao 1-0.