Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 10Article 584785

Soccer News of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Muguna, Mwamnyeto wabeba tuzo

Beki wa Yanga, Bakari Mwamnyeto Beki wa Yanga, Bakari Mwamnyeto

Mchezaji wa Azam Keneth Muguna ameibuka mchezaji bora wa mechi ya nusu fainali dhidi ya Yanga na kuzawadiwa Sh 1 milioni huku beki wa Yanga Bakari Mwamnyeto akiwa mchezaji aliyeonyesha uungwana akipewa Sh 300,000.

Katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Amaan, Azam imetinga fainali kwa kushinda penalti 9-8 baada ya dakika 90 kumalizika bila kufungana. Hivyo sasa anamsubiri mshindi kati ya Simba na Namungo mechi itakayoanza saa 2.15 usiku wa leo.

Hiyo ni tuzo ya pili kwa Muguna baada ya awali kushinda katika mechi ya makundi walipocheza na Namungo huku akiifungia timu yake bao la ushindi katika ushindi wa 1-0.

Hata hivyo zawadi hiyo ya Mchezaji Bora hatua ya fainali imeboreshwa ambapo atakayeibuka mshindi atajinyakulia Sh 2 milioni kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC) ambao ni wadhamini wa mashindano hayo.