Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 20Article 552634

Soccer News of Friday, 20 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Mukoko aruhusiwa!, Aucho na Bangala nao wamo

Kiungo wa Yanga, Mukoko Tonombe Kiungo wa Yanga, Mukoko Tonombe

Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema kiungo wa timu hiyo, Mkongomani Tonombe Mukoko bado ni mali ya Yanga ila hakuonekana mazoezini kwasababu nyota huyo hakuwa fiti yeye pamoja na mlinzi wa kati, Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

Bumbuli amesema, “Alikuwa na tatizo la kiafya ambalo lilimuweka nje yeye pamoja na Abdallah Shaibu 'Ninja' kwa siku tatu tangu wafike Morocco, lakini baada ya kufanyiwa tathmini leo ameruhusiwa kufanya mazoezi ya jioni pamoja na wenzake".

Baada ya Bumbuli kusema hayo, Mukoko mwenyewe amefunguka kwa kusema alikuwa anasumbuliwa na kichwa lakini kwa sasa yupo sawa na anaendelea na mazoezi. “Tumekuja hapa, nilikuwa naumwa kichwa kidogo, sasa hivi niko fresh mimi niko hapa na Yanga sasa hivi”.

Kwa upande mwingine, Kiungo mpya wa Wanajangwani, kutoka Uganda, Khalid Aucho anatazamiwa kujiunga na kambi leo Agosti 20, 2021 wakati beki Yennick Bangala atajiunga na kikosi hicho kilichopo Morocco kwa sasa siku ya Jumamosi ya kesho Agosti 21, 2021.