Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 22Article 558904

Soccer News of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Muonekano wa Azam Complex nyakati za usiku (+ Video)

Monekano wa Uwanja wa Azam Complex baada ya Kufanyiwa maboresho play videoMonekano wa Uwanja wa Azam Complex baada ya Kufanyiwa maboresho

Kuelekea Msimu wa 2021/2022 Klabu ya Azam FC, ambao ndio wamiliki wa Uwanja wa Azam Complex uliopo maeneo ya Chamazi Jijini Dar es Salaam, wamefanya maboresho makubwa katika uwanja huo ambayo yamegharimu takribani Bilioni 5.

Maboreshoo hayo ikiwa ni pamoja na kuweka nyasi bandia katika sehemu ya kuchezea na kuweka taa zenye ubora tofauti na zilizokuwepo awali.

Maboresho hayo ya uwanja wa Azam Complex yamekuwa na faida kubwa kwa Azam wenyewe na Taifa kwa ujumla kwani mechi nyingi za kimataifa kwa timu ambazo zinashiriki mashindano haya kwa hapa Tanzania zimekuwa zikichezwa hapa.

Hivi karibuni wakati wa Mechi za Ligi ya Mabingwa na zile za Kombe la Shirikisho ziliomba kuutumi uwanja wa Azam Complex kama Uwanja wao wa nyumbani ikiwa ni pamoja na Biashara United, Horseed FC ya nchini Somalia, Le Messager de Ngozi na Bunamuru FC kutoka Burundi.