Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 20Article 552700

Soccer News of Friday, 20 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mwalimu Kashasha kuzikwa August 23

Marehemu Alex Kashasha Marehemu Alex Kashasha

Mwili wa aliyekuwa mchambuzi mahiri wa kandanda hapa nchini, Mwalimu Alex Kashasha unatarajiwa kuzikwa Jumatatu Agosti 23 katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam.

Kashasha alifariki dunia Jana Agosti 19 katika hospital ya Kairuki Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya figo.

Akizungumza kwa niaba ya familia kaka wa marehemu Deus Kashasha amesema, mdogo wake atapumzishwa katika nyumba yake ya milele siku ya Jumatatu Agosti 23.

Deusi amesema ni uchungu mkubwa Kama familia kumpoteza mpendwa wao lakini ndiyo kazi ya Mungu haina makosa.

"Ndio hivyo tena mdogo wangu ametuacha tunamuombea kwa Mungu ampe pumziko la milele, "amesema Deusi.

Aidha Deus amesema kutokana  na umbali wa kwenda alikokuwa akiishi Mwalimu Kashasha kama familia wanatafuta eneo la karibu ili waombolezaji waweze kufika kuurahisi.

"Huku Mbagala Majimatitu ni mbali hivyo Kama familia tunatafuta eneo rafiki ambalo litakuwa na urahisi wa kila mpendwa wake kufika kumuaga mpendwa wao,

Amesema kutokana na maambukizi ya covid wanatamani zoezi hilo la kuaga lifanyike walau uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo ndio sehemu iliyomfanya kujulikana zaidi.

"Tunatamani sana uwanja wa Mkapa ambao ulimfanya kuwa maarufu sana Kama tukipata nafasi hapo tutafurahi sana itakuwa fursa kubwa kwa kila mpenda michezo kumshuhudia.

"Kama tukikosa nafasi tutaangalia namna gani ya kufanya Ila hapa nyumbani kwake ni padogo na hasa hili wimbi la Corona,"amesema Deusi.

Kashasha atakumbukwa kwa mengi hasa udambwidambwi wake akiwa anatangaza michezo ya ligi kuu Tanzania Bara.