Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 10Article 584641

Soccer News of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mwamuzi anusurika Kipigo, alitaka kumaliza mech kabla ya Muda

Chanzo ni kutaka kuzipeleka timu mapumziko kabla ya kukamilika dakika 45 Chanzo ni kutaka kuzipeleka timu mapumziko kabla ya kukamilika dakika 45

Mwamuzi Mudy Miliki jana manusura ajikute kwenye wakati mgumu alipoamua timu kwenda mapumziko kabla ya muda kufika katika mchezo wa fainali ya Ligi daraja la tatu mkoani Mbeya kati ya City Gold na Chemchem FC.

Tukio hilo lilitokea wakati ikiwa dakika ya 43 ambapo mwamuzi huyo alijikuta akipuliza firimbi akiashiria timu kwenda mapumziko na kuwafanya wachezaji na benchi la ufundi la Chemchem FC kumjia juu wakipinga maamuzi hayo na kufanya mechi kusimama kwa muda.

Hata hivyo mwamuzi wa pembeni (kibendera) Frank Sostenes kumuita refa huyo na kumuonesha kuwa muda haujaisha na mwamuzi huyo kuamuru mpira kuendelea ambapo City Gold walikuwa wakiongoza mabao 2-0 yaliyofungwa na James Ernest dakika ya 22 kwa penalti na 37.

Akielezea tukio la mwamuzi kusimamisha mchezo kabla ya muda, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (Mrefa), Lucas Kubaja amesema hali hiyo imemtokea kutokana na saa yake kujaa maji na kupoteza uhalisia na kwamba Ligi ilikuwa na mvuto japokuwa changamoto ilikuwa ni kukosa udhamini.