Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 17Article 543031

Michezo Mingine of Thursday, 17 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mwanza, Songwe zang’ara netiboli

Mwanza, Songwe zang’ara netiboli Mwanza, Songwe zang’ara netiboli

TIMU za netiboli za Mwanza na Songwe zimetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (Umitashumta) inayoendelea mkoani Mtwara.

Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Umitashumta, John Mapepele, Mwanza katika mchezo wake wa robo fainali uliochezwa jana, iliibuka na ushindi dhidi ya Morogoro wa magoli 85-20, huku Songwe ikiifunga Tanga magoli 36-29.

Kwa upande wa mpira wa mikono, Mwanza iliwafunga Pwani magoli 24-13, Rukwa iliifunga Manyara magoli 18-17 na upande wa wasichana, Morogoro iliwafunga Geita magoli 8-5 na Katavi iliifunga Singida magoli 11-6.

Katika mchezo wa mpira wa goli, Rukwa iliwafunga Mbeya magoli 13-12, Dodoma iliwafunga Mtwara magoli 18-4 na Tabora iliwafunga Singida magoli 14-6, huku kwa upande wa timu za wasichana, Tabora ikiwafunga Iringa 14-12 na Morogoro iliwafunga Singida 10-0.

Katika mpira wa wavu, Mwanza na Katavi kwa upande wa wanaume walishinda kila mmoja seti 3-0 dhidi ya Mbeya na Dar es Salaam, ambapo kwa wasichana Mtwara na Mbeya zilishinda seti 3-0, 3-1 dhidi ya Kilimanjaro na Mwanza.

Mchezo wa kurusha mkuki kwa wasichana waliofanya vizuri ni Devotha Mwaikra kutoka Manyara aliyerusha meta 31:00, Elizabeth Kelali kutoka Mara meta 29:82, Martha Samweli kutoka Manyara meta 28:35, Faustina Raphael kutoka Arusha meta 27:60 na Mariam Festo kutoka Pwani meta 25:70.

Kwa wavulana, Juma Gidawasi wa Manyara alirusha meta 42:80, Masanja Igoko kutoka Shinyanga meta 39:40, Masanja Malawa wa Singida meta 38:93, Masesa Juma kutoka Tabora meta 38:90 na Japhet Masunga kutoka Simiyu meta 38:50.