Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 14Article 585814

Mpira wa Kikapu of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

NBA: Antetokounmpo Ang’ara vs Warriors

Antetokounmpo Ang’ara vs Warriors Antetokounmpo Ang’ara vs Warriors

Burudani ya mchezo wa kikapu kunako Ligi ya NBA inaendelea! The Greek Beast, Giannis Antetokonumpo amekiwasha dhidi ya Golden State Warriors.

Milwaukee Bucks walikuwa uwanjani wakichuana na Warriors katika muendelezo wa NBA msimu huu. Giannis ameongoza vyema mashambulizi dhidi ya Steph Curry na wenzake.

Ushindi wa pointi 118-99 kwa Bucks ulichagizwa na ‘triple double” ya Antetokounmpo ambaye alifunga pointi 30, pasi 11 za magoli na kucheza mipira 12 iliyopotea. Upande wa pili, Stephen Curry alipachika pointi 12, pasi 4 za magoli na mipira 8 iliyopotea.

Matokeo ya michezo mingine ya NBA:

Denver Nuggets 140-108 Portland Trail Blazers, Brooklyn Nets 109-130 Oklahoma City Thunder, New Orleans Pelicans 113-89 Los Angeles Clippers na, Memphis Grizzlies 116-108 Minnesota Timberwolves