Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 24Article 544093

Habari za michezo of Thursday, 24 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

NYIE! Yanga waitangazia vita Simba

NYIE! Yanga waitangazia vita Simba NYIE! Yanga waitangazia vita Simba

LICHA ya kikosi chao kuruhusu mabao manne kwenye michezo miwili iliyopita ya Ligi Kuu Bara, mashabiki wa Yanga huko Morogoro sio wanyonge wakiwa vibanda umiza, unaambiwa wametoa tambo mbele ya watani zao na kuwaambia watakiona cha moto msimu ujao wa ligi hiyo.

Tambo hizo zilichukua nafasi wakati wakiufuatilia mchezo wao wa dhidi ya Mwadui, mtifuano huo wa maneno ulianza baada ya shabiki wa Simba kuwachokoza Yanga kwa kusema kwa ubovu wa chama lao mbona watasubiri sana maana walikuwa nyuma kwa mabao 2-1.

Unaambiwa mashabiki wa Yanga walichachamaa, kila mmoja alikuwa akimtupia dongo shabiki huyo wa Simba ambaye alikuwa akitamani kuona watani zake wakipoteza mchezo huo.

Ndipo Big mmoja, aliposema, “Nyie wenyewe mliwafunga kwa tabu, tutoleeni upuuzi wenu kwanza hii shoo haiwahusu sijui umefuata nini hapa, msimu ujao mtatueleza.”

Balaa lilikuwa zito kibandani hapo kwa mujibu wa shuhuda wetu maana baada ya Yanga kuchomoa bao ambalo walikuwa wametanguliwa na kufunga la ushindi, shabiki yule wa Simba alichomoka kama mshale mbio na kuondoka bandani maana wananchi walikuwa na vibe kama lote.