Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 20Article 547711

Habari za michezo of Tuesday, 20 July 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nabi, Gomes akili zote michuano CAF

Nabi, Gomes akili zote michuano CAF Nabi, Gomes akili zote michuano CAF

LIGI Kuu Bara imefikia tamati juzi kwa timu nne za Simba, Yanga, Azam na Biashara United kukata tiketi ya michuano ya kimataifa inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na makocha wa timu hizo wamefichua wameanza mipango mapema ili timu zao zifanye vizuri.

Simba iliyobeba ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo na Yanga iliyomaliza ya pili na zitakazokutana katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) zitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Azam na Biashara zikicheza Kombe la Shirikisho Afrika.

Michuno yote inaanza Septemba 11 na makocha wa timu hizo wamesema baada ya kumalizika kwa ligi kwa sasa akili zao wamezielekeza kwenye michuano hiyo ya CAF ili kuhakikisha zinafanya vizuri ili kulinda nafasi nne ilizopata Tanzania msimu huu baada ya Simba kung’ara Afrika.

Wakizungumza na Mwanaspoti kwa muda tofauti, makocha wa timu hizo, Didier Gomes wa Simba, Nasreddine Nabi wa Yanga, George Lwandamina wa Azam na Patrick Okumu wa Biashara kila ammoja amejinasibu kujipanga zaidi kwa ajili ya michuano hii.

Gomes alisema timu kikosi chake kipo vizuri na amepanga kufanya mabadiliko kidogo kuelekea kimataifa msimu ujao.

“Msimu ulioisha wikiendi tuliishia robo fainali, tunahitaji kufika mbali zaidi na tutajipanga kwa msimu ujao,” alisema.