Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 26Article 553795

Habari za michezo of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nabi: Tunaanza upya nyie subirini

Nabi: Tunaanza upya nyie subirini Nabi: Tunaanza upya nyie subirini

KOCHA mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi ametua nchini jana na kutamka kwamba bado hajapata muunganiko katika timu yake licha ya kuwa nchini Morocco kwenye maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

Yanga iliweka kambi nchini Morocco kwa takribani wiki moja na sasa wamerejea nchini, kundi la kwanza Yanga liliwasili jana jioni Uwanja wa Julius Nyerere Terminal 3 na wachezaji waliokuwa wanaenda kambi ya Taifa Stars walipanda gari ndogo na kuachana na wenzao waliokwenda kambini Avic Town.

Akizungumza na waandishi wa habari, Nabi alisema; “Muunganiko wa timu bado, tunahitaji muda kama mwezi au miezi mitatu kwa sababu timu haijengwi kwa muda mfupi, tuna wachezaji wa zamani na wapya na wanahitaji kuwa sawa. Wachezaji wote tuliowasajili ni wazuri kwa sababu tulikuwa tunawafuatilia, tukipata muda zaidi tutakuwa bora zaidi,” alisema Nabi

Naye mshambuliaji Saido Ntibazonkiza alisema; “Kama kocha alivyosema muda ulikuwa mchache lakini tukiunganika vizuri tutakuwa bora zaidi, kikosi kipo vizuri.”

Wakati huo huo. Mjumbe wa Kamati ya Mashindano Yanga, Injinia Hersi Said alisema wamemaliza usajili na kuhusu Siku ya Wananchi alisema; “Maandalizi yanaendelea vizuri na tunaamini kabisa itakuwa bora zaidi ya miaka ya nyuma.”

SIMBA WATUA

Nyota wa Yanga walitua pamoja na wale wa Simba ambao wanajiunga na kambi ya Stars ambao ni Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein na Israel Patrick.