Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 04Article 545200

Habari za michezo of Sunday, 4 July 2021

Chanzo: dar24.com

Nabi afichua mbinu zilizoikwamisha Simba SC

Nabi afichua mbinu zilizoikwamisha Simba SC Nabi afichua mbinu zilizoikwamisha Simba SC

Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreedine Al Nabi, amefichua mipango iliyomuwezesha kuifunga Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo Jumamosi (Julai 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Nabi amefichua mpango huo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kikosi chake kumaliza kazi ya kukusanya alama tatu dhidi ya Mtani.

Kocha huyo kutoka nchini Tunisia amesema: “Simba ni timu nzuri tulichokifanya ni kuwasoma ubora wao ili kuwazuia na mapungufu yao ili kuwafunga na tumefanikiwa.

“Wachezaji wangu wamejitahidi kuyafanyia kazi malekezo tuliyowapa. Tutafurahia kwa muda mfupi kabla ya kujiandaa na mchezo wa fainali baadae mwezi huu, tunajua watakuja kwa nia ya kulipa kisasi ndio maana tunapaswa kujipanga.”

Kwa ushindi wa bao 1-0, Young Africans imefikisha alama 70 ambazo zinaendelea kuiweka katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Simba SC inaendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kusaliwa na alama 73, huku ikijipanga kucheza mchezo ujao dhidi ya KMC FC Julai 07, Uwanja wa Benjamin Mkapa.