Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 07Article 541444

Habari za michezo of Monday, 7 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Nabi ahofia afya ya Tonombe

Nabi ahofia afya ya Tonombe Nabi ahofia afya ya Tonombe

KUUMIA kwa kiungo Tonombe Mukoko wa Yanga, kumempa hofu kocha mkuu wa timu hiyo Nasreddine Nabi, ambaye amesema ni mchezaji anayemtegemea katika mechi zilizosalia za msimu.

Mukoko alishindwa kuendelea na mchezo juzi baada ya kuumia mapema wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, iliyokuwa ikicheza na Tunisia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambao Congo walifungwa bao 1-0.

Akizungumza na gazeti hili Nabi, alisema kuumia kwa kiungo huyo kumempa hofu kwa sababu ni mchezaji ambaye amempa majukumu maalumu katika mechi zilizosalia za ligi na michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambazo ni muhimu kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri katika kutwaa mataji hayo.

“Bado sijajua ukubwa ya maumivu aliyonayo lakini inanipa hofu kama majeraha hayo yatamzuia kucheza na nasubiria taarifa ya daktari wa timu yake ya Taifa na baada ya kujua ukubwa tutajua, tutafanyaje,” alisema Nabi ambaye ameonesha kuvutiwa na kiungo huyo.

Kocha huyo alisema amekuwa akiwafuatilia kwa karibu wachezaji wake wote walioitwa timu za taifa lengo ni kutaka kujiridhisha na ufanisi wao na namna wanavyowajibikaji wanapokuwa na timu zao za taifa na ameridhika ingawa amekuwa akihofia kupata majeraha.

Alisema anachotaka ni kuona wachezaji wanarudi kujiunga na wenzao wakiwa na viwango vyao kama walivyoondoka ili kuweka uwiano ambao utasaidia kufikia malengo ya kushinda mechi na kutwaa ubingwa kama ambavyo wamekusudia

Nabi alisema anajua presha ni kubwa kwa mashabiki lakini yeye na wenzake wamezipa umuhimu mechi ambazo zimesalia na kuhakikisha wanarudisha tabasamu la mashabiki kwa kuwapa mataji ambayo wamekusudia kubeba msimu huu.

Yanga imesalia na mechi tano kabla ya kumaliza msimu kwenye ligi wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi 61 na vinara ni Simba ikiwa na pointi 67 katika mechi 27 walizocheza.

Yanga imetinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la ASFC ambapo sasa itapambana na Biashara United ya Mara na Simba ikicheza Azam FC.

Join our Newsletter