Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 559891

Soccer News of Monday, 27 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nabi bado yupo sana Yanga

Kocha wa Yanga Nabi, wa Pili kushoto Kocha wa Yanga Nabi, wa Pili kushoto

Mabosi wa Yanga wamekunjua roho na kusema wazi kuwa, hawana mpango kabisa wa kuachana na kocha wao Nasreddine Nab, huku wakisisitiza kuongezwa kwa Cedric Kaze ni lengo la kubioresha benchi lao la ufundi ili kuwa na wataalamu wa kutosha.

Kauli ya mabosi wa Yanga imetoka saa chache baada ya Nabi na Kaze kuiwezesha Yanga kutwaa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Simba bao 1-0 katika mechi kali iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar.

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said ameliambia Mwanaspoti kuwa, wanatambua uwezo wa Nabi kumuongezea msaidizi sio jambo la kumtafutia njia ya kuondoka kama wengi wanavyobashiri, ila lengo ni kuhakikisha wanakuwa bora kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji.

“Ushindi tulioupata leo ni nguvu tulizowekeza kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji, yanazungumzwa kutokana na ujio wa Kaze naweza kusema kama wanasubiri Nabi aondoke watasubiri sana, ila ni kwamba wajiandae kuona benchi bora la makocha wasomi wakifanya kazi pamoja,” amesema.

Kuhusu ushindi wao, amesema analipongeza benchi la ufundi na aliyependekeza usajili wa kipa wao namba moja Diarra Djigui kuwa ameitendea haki nembo ya timu.