Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 13Article 585367

African Cup of Nations of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Nahodha wa Burkina Faso akutwa na Covid-19, kuikosa Cape Verde

Bertrand Traore Bertrand Traore

Nahodha wa timu ya taifa ya Burkina Faso Bertrand Traore atakuwa nje ya kikosi hicho kwenye mechi ya pili ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 baada ya kubainika kuwa na dalili za maambukizi ya virusi vya Covid-19 dhidi ya Cape Verde.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alikiongoza kikosi hicho kwenye mtanange wa ufunguzi wa mashindano hayo dhidi ya Cameroon ambapo walikumbana na kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Cameroon Jumapili.

Inaelezwa pia kuwa mchezaji huyo anaweza kukosa hata mchezo wa mwisho wa Kundi A dhidi ya Ethiopia utakaopigwa Januari 17.

Issoufou Dayo atakuwa nahodha kufuatia kukosekana kwa Traore.