Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 25Article 544180

Habari za michezo of Friday, 25 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Namungo, Azam kuamua hatma ya Ruvu Shooting

Namungo, Azam kuamua hatma ya Ruvu Shooting Namungo, Azam kuamua hatma ya Ruvu Shooting

Ligi Kuu Tanzania Bara imeendelea leo ambapo Ruvu Shooting waliokuwa katika uwanja wa nyumbani kucheza dhidi ya Polisi Tanzania ambao wao wanauhakika wa kubaki katika ligi.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1, huku Ruvu Shooting waliokuwa nyumbani ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa David Uromy ambaye anafunga mechi ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo katika mechi iliyopita dhidi ya Yanga kabla ya kipindi cha pili, Tariq Seif wa Polisi kusawazisha.

Kutokana na matokeo hayo Polisi Tanzania wameongeza pointi moja na kwenda mpaka nafasi ya saba wakiwa na pointi 42, wakati Ruvu Shooting wao bado hali si shwari kwani wapo nafasi ya 10 wakiwa na pointi 38, ambazo zinaweza kufikiwa na Coastal Union ambao wapo nafasi ya pili kutoka mkiani.

Ili Ruvu Shooting waweze kusalia katika ligi msimu huu wanahitaji kushinda mechi mbili ngumu ambazo zote watacheza ugenini dhidi ya Namungo na Azam ambao wote wawili hawa wanapambana kusaka pointi tatu ili kumaliza katika nafasi nne za juu.