Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 18Article 552244

Soccer News of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Nani aanze, nani asubiri Simba SC

Kikosi cha Simba kikiwa Mazoezini, nchini Morocco walikokwenda kuweka Kambi Kikosi cha Simba kikiwa Mazoezini, nchini Morocco walikokwenda kuweka Kambi

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes atakuwa na kibarua kigumu katika kupanga kikosi chake cha kwanza katika msimu ujao.

Hiyo ni kutokana na usajili babkubwa uliofanywa wa wachezaji wapya katika kutengeneza kikosi imara watakachokitumia katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Simba hadi hivi imefanya usajili wa wachezaji saba katika kukiboresha kikosi chao ambao wa kigeni ni Pape Ousmane Sakho (Mali), Enock Baka (Congo) anayesubiria kutamburishwa, Duncan Nyoni na Peter Banda (Malawi).

Wachezaji wazawa ni Jeremiah Kisubi (Tanzania Prisons), Kibu Denis (Mbeya City) Yusuf Mhilu (Kagera Sugar) na Ezrael Mwenda (KMC FC).

Katika msimu ujao kikosi cha kwanza kinatarajiwa kuwa na mabadiliko makubwa kutokana na usajili huo unaoendelea kufanywa katika kujiimarisha zaidi.

Mabadiliko hayo yanatokana na wachezaji wao wawili waliouzwa Mzambia Clatous Chama na Luis Miquissone kutoka Msumbiji.

Kikosi kinatarajiwa kuwa hivi, kipa ni Kisubi ambaye amesajiliwa kwa ajili ya kumpa changamoto Aishi Manula aliyekuwa katika kiwango bora hivi sasa.

Beki wa kulia ni Ezrael mwenye nafasi kubwa ya kuingia katika kikosi cha kwanza mbele ya mkongwe Shomari Kapombe. Beki wa kushoto ataendelea kucheza Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kutokana na kutosajili mchezaji katika nafasi hiyo anayocheza na Gadier Michael.

Namba nne ni Baka aliyesajiliwa maalum kwa ajili ya kucheza pamoja na Joash Onyango ambaye yeye atacheza tano. Baka ataingia moja kwa moja katika kikosi hicho akimuondoa Pascal Wawa.

Kiungo mkabaji namba sita Taddeo Lwanga ataendelea kucheza nafasi hiyo huku saba akicheza Banda akicheza nafasi ya Luis anayetarajiwa kusajili Al Ahly ya Misri wiki hii na kiungo mchezeshaji nane atacheza Kanoute atakayemuondoa Raly Bwalya ambaye msimu uliopita hakuwa anapata nafasi sana katika kikosi cha kwanza.

Mshambuliaji wa kati namba tisa, atacheza Kibu ambaye ana kibarua kigumu cha kupambana zaidi ili amtoe nahodha John Bocco.

Namba kumi ni Sakho anayemudu kucheza nafasi pia za winga 7 na 11. Yeye anaingia kuchukua nafasi ya Chris Mugalu huku 11 akicheza Duncan ambaye anaingia kikosini baada ya Chama kuuzwa Berkane.