Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 08Article 584326

Soccer News of Saturday, 8 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Napoli Watangaza Rasmi Kumsajili Axel Tuanzebe

Ukaribisho wa Tuanzebe ndani ya Napoli Ukaribisho wa Tuanzebe ndani ya Napoli

Napoli wametangaza rasmi Axel Tuanzebe kuwa amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo wa miezi sita akitokea Manchester United na anaweza kucheza mechi yake ya kwanza kesho dhidi ya Sampdoria.

Beki huyo wa kati alikuwa Naples mapema wiki hii kwa matibabu yake na kutia saini kandarasi, kisha akarejea Uingereza kukamilisha ombi la visa.

Hii ni kwa sababu baada ya sheria za Brexit, sheria ya kusaini na kucheza soka kwa Uiingereza ni tofauti na wanachama wa EU.

Tuanzebe amewasili kwa mkopo wa miezi sita hadi Juni 30, 2022, bila chaguo la kumnunua.

Alikuwepo kwa mkopo Aston Villa hadi msimu huu, lakini mkataba ulivunjwa kwa makubaliano baada ya Napoli kuwasilisha ofa.

Sasa ni suala la muda tuu ili Tuanzebe asajiliwe na kuwa tayari kuwa sehemu ya kikosi cha Napoli dhidi ya Sampdoria kwa mchezo wa Jumapili wa Serie A.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kimsingi ni beki wa kati, lakini pia anaweza kucheza nafasi ya beki wa kulia inapohitajika.