Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572395

Soccer News of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nchimbi aenda kuongeza nguvu Geita

Ditram Nchimbi Ditram Nchimbi

Baada ya kumalizana na Yanga, Mshambuliaji Ditram Nchimbi amejiunga na klabu ya Geita Gold inayoshiriki Ligi Kuu kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Nchimbi ambaye alijiunga na Yanga Desemba 19 2019 ameitumikia timu hiyo miaka miwili baada ya kuona mambo yake sio mazuri ndani ya timu hiyo ameamua kujiengua mwenyewe.

Nyota huyo wa zamani wa Azam, Mwadui na Polisi Tanzania alisepa Yanga baada ya mkataba wake kumalizika na uongozi kutoonyesha nia ya kumuongeza mkataba huku akiwa hana nafasi kubwa kwenye kikosi cha kocha Nasredinne Nabi.

Akizungumza Katibu wa Geita Gold, Revinus Ntare amesema wamemnasa mshambuliaji huyo kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo anatarajiwa kujiunga na kikosi hicho baada ya mwezi mmoja.

Amesema lengo ni kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji inayoongozwa na Juma Mahadhi, Salim Aiyee na Danny Lyanga ambayo haijaonyesha makali kwenye mechi zao tano za msimu huu ikiwa imefunga mabao mawili tu katika mechi tano.

“Ni kweli tumemsajili Nchimbi kwa mkataba wa mwaka mmoja atajiunga na timu baada ya mwezi mmoja dirisha dogo likifunguliwa, naamini ataleta nguvu mpya ndani ya kikosi na kuichangamsha safu ya ushambuliaji,” amesema Ntare.

Mdau wa soka mjini Geita, Pius Kimisha alisema usajili huo ni mzuri kwa kikosi hicho ambacho hakijawa na makali hu