Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 08Article 546040

Habari za michezo of Thursday, 8 July 2021

Chanzo: dar24.com

Ndoto za ubingwa Young Africans bado zipo

Ndoto za ubingwa Young Africans bado zipo Ndoto za ubingwa Young Africans bado zipo

Uongozi wa klabu ya Young Africans umethibitisha kuwa tayari wamewasilisha ushahidi wa kesi dhidi ya mchezaji Bernard Morrison na kinachosubiriwa sasa ni kutolewa hukumu kwa kesi hiyo

Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa Michezo (CAS) inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi hiyo kabla ya mwezi huu kumalizika

Mapema wiki hii katika mahojiano na Azam TV, Afisa Habari wa Young Africans Hassan Bumbuli alitamba kuwa watakuwa mabingwa msimu huu na jambo hilo litatokea kabla ya Julai 25 siku ya mchezo wa fainali kombe la FA.

“Tuna michezo miwili kukamilisha msimu, Julai 14 tutacheza na Ihefu Fc na Julai 18 Dodoma Jiji, tunahitaji kushinda mechi zote mbili. Naamini tutakuwa mabingwa msimu huu, tena jambo hilo litatimia kabla ya mchezo wa fainali ya FA,” alitamba Bumbuli

Inaelezwa kesi hiyo itatolewa maamuzi na CAS Julai 22 na Jaji kutoka nchini Uingereza.