Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 12Article 585307

Soccer News of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Newcastle United Kumsajili Chris Wood

Chris Wood Chris Wood

Newcastle United wapo kikazi zaidi chini ya utawala mpya. Huko sokoni, wanafanya makubwa. Chris Wood kutua St James’ Park leo!

Newcastle wamejikuta wakilazimika kusajili mshambuliaji kwenye dirisha hili baada ya Callum Wilson kupata majeruhi ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa muda. Kumkosa Wilson sambamba na hali ilivyo kwenye timu hiyo msimu huu, ni vitu ambavyo uongozi wa klabu hiyo hauwezi kuvivumilia.

Katika kuonesha kwa vitendo kuwa “they mean business”, Newcastle United wamegonga milango kule Turf Moor na sasa, wamevunja mkataba wa Chris Wood na Burnley. Wood alikuwa na kipengele cha dau la Pauni milioni 20 kwenye mkataba wake na Burnley.

Kipengele hiki kimewapa nguvu The Magpies ambao wamelipa pesa hiyo ili kumpata Wood kwenye dirisha hili. Kwa sasa, Chris Wood atafanyiwa vipimo vya afya na kisha kutangazwa kama mchezaji mpya wa Newcastle United leo leo.