Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 29Article 554227

Soccer News of Sunday, 29 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ni "Sapraizi" za Dunia kilele wiki ya Mwanachi

Mashabiki wa Yanga SC Mashabiki wa Yanga SC

Leo ni Agosti 29, Macho na masikio yote kwa Mkapa kushuhudia lile tukio la kihistoria la Kilele ya Wiki ya Mwananchi ambalo lilizinduliwa tangu Agosti 22 kule Zanzibar.

Wananchi ndani ya wiki nzima hii walijishughulisha ama kujihusisha na shughuli mbali mbali za kijamii kama njia ya kuadhimisha wiki hii lakini leo ndio leo pale kwa Mkapa.

Tukio kubwa ni Perfomance kutoka kwa wasanii mbali mbali wa kitaifa na kimataifa watakaoshusha burudani kuinogesha siku hiyo bila kusahau mwanamuziki nguli Mwenye asili ya Congo, Koffi Olomide atawarusha Wananchi.

Wakati hayo yakisubiriwa Mashabiki wa Yanga watasubiri tukio la lipekee la utambulisho wa nyota wao wapya waliosajiliwa msimu huu, tukio hilo likisindikizwa na Burudani mujarabu kwa mechi kati ya Yanga na Timu ya Zanaco kutoka kule nchini Zambia.

Wakati tukitazamia kuwa siku ya Mwananchi ndio itakua imefika tamati, Msemaji wa Yanga "Bugati" Haji Manara anatwambia ndio kwanza shughuli zitakua zinaanza, kutakua na Sapraizi ya Dunia siku ya Mwanachi kikubwa na cha msingi ni kila mmoja afike kwa Mkapa kujionea nini kinakwenda kuandikwa katka Historia ya Klabu hiyo Kongwe nchini.