Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 07Article 555760

Soccer News of Tuesday, 7 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ni Simba vs TP Mazembe Septemba 19 kwa Mkapa

Beki wa Simba, Mohamed Hussein akiwatoka wachezaji wa TP Mazembe Beki wa Simba, Mohamed Hussein akiwatoka wachezaji wa TP Mazembe

Klabu ya wekundu wa Msimbazi, Simba SC itawashusha wababe kutoka DR Congo, wakati wa maadhimisho ya tamasha la Simba, "Simba Day" linalotarajiwa kufanyika Septemba 19 katika Uwanja wa Mkapa Dare es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa na Wekundu wa msimbazi ili kukata kiu ya mashabiiki wao waliokuwa na hamu ya kujua Simba itacheza na nani katika kilele cha Tamasha la Simba.

TP Mazembe ni moja ya klabu kubwa barani Afrika ambapo wameshachukua ubingwa wa Afrika,Ubingwa wa Kombe la shirikisho na Ubingwa wa Ligi kuu Congo.

Kuna watanzania kadhaa waliowahi kupita katika klabu hiyo akiwemo Mbwana Samatta kabla ya kutimkia Ulaya, Thomas Ulimwengu na Ramadhan Singano "Messi".

Simba kwa sasa imeweka Kambi yake kule Jijini Arusha ikijifua kwa maandalizi ya msimu ujao.

Hivyo katika kilele cha "Simba day" itakuwa ni Vita ya wababe kutoka Tanzania na wababe kutoka Congo.