Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 28Article 560155

Soccer News of Tuesday, 28 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ni vita ya matajiri usiku wa UEFA

Kuelekea mchezo wa PSG vs Man City Kuelekea mchezo wa PSG vs Man City

Klabu ya Soka ya PSG, Usiku wa leo itaikaribisha Manchester City katika muendelezo wa michezo ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya hatua ya Makundi.

Mchezo huo wa Kundi A, ambao utapigwa katika dimba la Parc De Princes nchini Ufaransa, unatarajiwa kuwakutanisha vilabu ambayo vina thamani kubwa katika vikosi vyao barani Ulaya kwa sasa, na ndivyo ambavyo vimefanya usajili wa gharama ndani ya miaka mitano iliyopita.

Wote wawili wana kiu kubwa ya kuhakikisha wanaandika historia ya kubeba Kombe hilo la Ulaya ambalo licha ya mafanikio ya Klabu zote hizo mbili hakuna aliewahi kunyakua ubingwa huo.

Kivutio kikubwa katika mchezo huo ni kumuona Kocha Pep Guardiola kwa mara nyingine akikutana na nyota Lionel Messi ambae alikua akimtumia kuumiza wapinzani.

Messi na Pep Guardiola wamewahi kufanya kazi pamoja wakati messi akichezea barca na Pep akifundisha Barcelona.