Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 25Article 553558

Soccer News of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Nimejiunga na timu ambayo itashinda kila kikombe msimu ujao" - Manara

Haji manara (alievaa jezi ya kijani) akitambulishwa na Viongozi wa Yanga Haji manara (alievaa jezi ya kijani) akitambulishwa na Viongozi wa Yanga

Aliekuwa Afisa habari wa klabu ya Simba SC, Haji Manara amesema baada ya kuachia nafasi yake ndani ya Simba alipata ofa kutoka katika klabu mbali mbali nchini zilizokua zikimuhitaji akafanye nao kazi lakini yeye alitazama mipango husika ya kila timu.

Haji amesema katika upembuzi wake ametambua kuwa klabu ya Yanga ina mipango thabiti kuanzia usajili na namna ya uendeshaji hivyo yupo sehemu sahihi na salama katika maisha yake ya soka, kwani kwa kila hali kombe la Ligi kuu msimu ujao linakwenda Jangwani.

"Nimejiunga na Mabingwa mara 27 ambao wanakwenda kubeba kila kikombe msimu ujao, kwa kushirikiana na hawa wenzangu (Bumbuli na Nugaz) kwa kunihitaji wenyewe inaonekana ni kiasi gani wanatambua thamani yangu". amesema Manara

"Wanayanga niwaambie tu kuwa hii ni klabu kubwa, hatuna haja ya kulalamikia marefa, TFF, bodi ya ligi twendeni tukafanye kazi, hii ndio klabu kubwa Afrika Mashariki na kati" amesisitiza Manara

Haji Manara ametambulishwa mbele ya Viongozi wa Yanga kama msemaji mpya wa Klabu ya Yanga, na katika utambulisho huo Haji aliongozana na Familia yake ambao nao wamejiunga rasmi na klabu ya Yanga.