Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 07Article 541381

Habari za michezo of Monday, 7 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Ninja: Nacheza kwa ushauri wa Zlatan Ibrahimovic

Ninja: Nacheza kwa ushauri wa Zlatan Ibrahimovic Ninja: Nacheza kwa ushauri wa Zlatan Ibrahimovic

Dar es Salaam. Beki wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amesema timu yake imechangia kiasi kikubwa kipaji chake kujulikana ndani na nje, huku ushauri wa nyota wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic ukimwongoza.

Ninja alisajiliwa kwa mara ya kwanza na Yanga 2017 akitokea Taifa Jang’ombe ya Zanzibar, baadaye alipata ofa ya kwenda kuichezea MFK Karvina ya Jamhuri ya Czech ya Ligi Daraja la Tatu, ambayo ilimtoa kwa mkopo wa mwaka mmoja LA Galaxy ya Ligi Kuu ya Marekani.

Baada ya kutimuliwa kwa kocha Cesric Kaze, Ninja alianza kupata nafasi ya kucheza sambamba na Dickson Job hadi alipokuja kocha mpya, Mohammed Nabi, lakini kwa sasa ni majeruhi.

Kitu ambacho Ninja hakisahau kabisa katika maisha yake ya soka, kwamba kupitia Yanga alikukutana na nyota mkubwa duniani, Ibrahimovic, ambaye alibadilishana naye mawazo ya namna anavyotakiwa kufanya kazi yake kimamilifu na akawa mtu tofauti.

Alisema jambo kubwa analolikumbuka aliloambiwa na Ibrahimovic ni kwamba anatakiwa akiamini kipaji chake, kisha akifanyie kazi kwa bidii, akizingatia nidhamu ya kazi bila kushurutishwa na mtu.

“Yanga ina historia ya aina yake katika maisha yangu, kwani imekitangaza kipaji changu pakubwa sana, imenifanya nikutane na watu mbalimbali wakubwa duniani kama Ibrahimovic, ambaye aliniambia kitu kikubwa sana namna ya kuwa mchezaji wa kuona mbali.

“Ndiyo maana ilikuwa rahisi kurejea kwenye kikosi hicho baada ya kutoka nje ambako mwaka jana kulikuwa na mtikisiko wa ugonjwa wa covid 19, kwani niliona ni kama narudi nyumbani,” alisema.

Akizungumzia ushindani wa msimu huu, Ninja anaamini timu yao (Yanga) ni bora na kwamba itakuwa na ushindani mkali ambao mbele ya safari hakuna timu ambayo inaweza ikawayumbisha kupata matokeo.

“Ni msimu mgumu, lakini kila timu inapambana kwa malengo yake, ninachoamini Yanga ninayoijua mimi ipo siku itakuwa mwiba kwa kila timu kwani kila jambo lina wakati wake na mapito yake,” alisema.

Join our Newsletter