Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 25Article 559582

Soccer News of Saturday, 25 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ninja ana silaha zote za Nabi

Ninja na Nabi wakipeana maelekezo Ninja na Nabi wakipeana maelekezo

Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi kaamua kumpa mbinu zote za kiufundi beki kisiki Abdu Shaibu Ninja katika suala la kukabiliana na washambuliaji wa Simba.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumamosi hii saa kumi na moja jioni kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Safu ya ushambuliaji ya Simba inatarajiwa kuongozwa na Denis Kibu, Chris Mugalu na John Bocco ambao huenda wakakutana na Ninja anayecheza soka la jihad na undava.

Mmoja wa mabosi kutoka ndani ya benchi la ufundi la Yanga, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, kocha Nabi ameonekana akimpa mbinu na maelekezo ya jinsi ya kuwadhibiti washambuliaji katika mazoezi yake.

Juzi beki huyo alianzishwa katika kikosi cha kwanza kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya DTB inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza aliyecheza pamoja na Yannick Bangala Litombo.

Ameongeza kuwa upo uwezekano mkubwa wa Ninja kuanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii akicheza pamoja na Litombo.

“Kocha Nabi anaendelea kuboresha katika kila nafasi kwa kubadilisha wachezaji kwa lengo la kutengeneza kikosi imara kitakacholeta ushindani.

“Juzi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya DTB alionekana kuwabadilisha akina Mwamnyeto (Bakari) na Job (Dickson) kwa lengo la kuwaangalia Litombo na Ninja.

“Kikubwa anataka kuona safu ya ulinzi ikiwa imekamilika huku ikizuia hatari golini kwetu, hivyo kocha Nabi amevutiwa na Ninja, Litombo jinsi walivyocheza,” amesema bosi huyo.

Akizungumzia hilo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema: “Hilo ni suala la kiufundi, siyo sawa kulizungumzia nitakuwa kama ninaingilia majukumu ya kocha, hivyo ni vema tukamuachia kocha ambaye anajua mchezaji yupi yupo fiti kwa ajili ya mchezo huo.”