Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 22Article 552910

Soccer News of Sunday, 22 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Niyonzima apongeza usajili Yanga

Haruna Niyonzima Haruna Niyonzima

Aliekuwa kiungo fundi wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema kwa usajili unaofanywa na Yanga katika dirisha hili la usajili ni bab kubwa na wanakwenda kufanya mambo makubwa.

Yanga kwa misimu minne sasa wamelikosa taji la Ligi kuu na hivyo wanapambana kila hali kuhakikisha wanalinyakua msimu ujao.

Kwa mujibu wa Niyonzima, Yanga itakuwa bora zaidi msimu ujao endapo wachezaji watapata muunganiko wa mapema na hasa ikizingatia timu imekuwa mpya kwa asilimia kubwa.

"Usajili wamejitahidi sana japokuwa wengi wao ni wapya ila wakikaa sawa watakuwa bora sana msimu ujao," anasema Niyonzima.

Anasema kwa namna ambavyo wanajiandaa huko walipo kabla ya ligi kuanza, watafanya makubwa na kuzidisha ushindani hata katika michuano ya Kimataifa ambapo Yanga inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Niyonzima licha ya kuachwa ndani ya kikosi hicho uongozi ulithamini mchango wake na kumuaga kwa heshima kubwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.