Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 10Article 584542

Tennis News of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Novac Djokovic ashinda Mahakamani, aruhusiwa kusalia nchin Australia

Mcheza Tennis, Novac Djokovic Mcheza Tennis, Novac Djokovic

Mahakama imeamua kwamba Novak Djokovic ataachiliwa huru, baada ya hakimu kukuta hakuna msingi wowote katika mamlaka nchini Australia alivyofanya uamuzi wake wa kufuta visa ya nyota huyo wa mchezo wa tenisi.

Mahakama ilisimamisha vikao kwa muda mrefu baada ya mawakili wa serikali kuwasilisha ufunguzi wao.Sasa ni wazi kwamba kuahirishawa huko ndiko wakati ambapo serikali iliondoa kesi yao.

Jaji Anthony Kelly ameamua kwamba agizo la kughairi visa ya Djokovic "limefutwa" mara moja.Hii inamaanisha kuwa visa yake sasa ni halali na anaweza kuingia nchini Australia.