Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 24Article 544072

Habari za michezo of Thursday, 24 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Nyoni kununulia mashabiki 50 tiketi

Simba na Azam FC, zitashuka uwanjani hapo Jumamosi na mshindi atakutana na mshindi wa nusu fainali ya kwanza kati ya Yanga na Biashara United itakayopigwa kesho, Ijumaa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Akizungumza na mwandishi wetu kabla ya jana kuelekea Songea kwa ajili ya mchezo huo, Nyoni alisema ni mwenye furaha kurejea nyumbani kwao, Songea kucheza tena katika Uwanja wa Majimaji baada ya muda mrefu.

"Ni muda mrefu sijacheza katika uwanja wa nyumbani, Songea tangu Majimaji ishuke daraja, hivyo nitatoa zawadi kwa mashabiki kwa kuwanunulia tiketi 50 kuingia kuishuhudia mechi yetu dhidi ya Azam," alisema Nyoni ambaye Songea ni nyumbani kwa wazazi wake.

Simba ilitua Songea jana na kupokewa na umati wa mashabiki waliondamana na basi la timu hiyo lililowapokea kuanzia uwanja wa ndege hadi katikati ya mji.