Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 30Article 560629

Soccer News of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Nyota Dodoma Jiji awatisha Simba

Wachezaji wa Dodoma wakishangilia goli dhidi ya Ruvu Shooting Wachezaji wa Dodoma wakishangilia goli dhidi ya Ruvu Shooting

Mchezaji wa Dodoma Jiji, Cleophance Mkandala ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba ambao utakuwa ni wa mzunguko wa pili, utakaopigwa Oktoba 1.

Dodoma Jiji imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mtupiaji wa bao hilo alikuwa ni Mkandala mwenyewe aliyepachika bao lake la kwanza kwa msimu wa 2021/22 na kuipa pointi tatu muhimu.

Mkandala amesema:"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Simba na kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu," .

Simba ipo Dodoma imetoka kugawana pointi mojamoja na Biashara United katika mchezo wa mzunguko wa kwanza.