Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 25Article 553642

Soccer News of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nyota Simba, Yanga waanza tizi Stars

Wachezaji wa Taifa Stars wakiendelea na mazoezi Wachezaji wa Taifa Stars wakiendelea na mazoezi

Nyota wa klabu za Simba na Yanga wameungana na kikosi cha Stars kinachofanya mazoezi leo asubuhi katika uwanja Uhuru, Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu hizo walikuwa wameweka kambi nchini Moroccco wakijiandaa na Ligi Kuu lakini jana walirejea na moja kwa moja wamejiunga na wenzao katika mazoezi ya kwanza leo asubuhi.

Mwanaspoti limewashuhudia  wachezaji wa Simba,Aishi Manula, Israel Patrick, Erasto Nyoni,Mzamiru Yassin, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein na Kennedy Juma huku mshambuliaji John Bocco ikielezwa amebaki kambini (Stars)  hali yake ikiwa sio nzuri.

Upande wa Yanga wachezaji waliokuwepo kwenye mazoezi ni Ramadhan Kabwili, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Feisal Salum na Zawadi Mauya.

Wakati upande wa wachezaji wa Azam ambao hawakwenda kambini nchini Zambia kwa sababu ya Stars ni Ayoub Lyanga, Salum Abubakary, Mudathir Yahya, Lusajo Mwaikenda, Idd Seleman, Edward Manyama na Wilbol Maseke.

Wengine waliokuwepo katika mazoezi ni Metacha Mnata, Abdul Suleiman (Coastal Union) na Meshack Abraham(Kagera Sugar).

Stars inajiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la Dunia nchini Qatar dhidi ya DR Congo utakaopigwa Septemba 2, DR Congo.