Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 28Article 554122

Soccer News of Saturday, 28 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Nyota wa Yanga waliobaki Morocco kutua leo

Kikosi cha Yanga Kikosi cha Yanga

Nyota wa Yanga ambao walibaki nchini Morocco wanatarajiwa kurejea Tanzania leo ili kuungana na timu katika maandalizi ya msimu wa 2021/21.

Sababu ya nyota hao kukwamwa inatajwa kuwa ni kushindwa kukamilisha masuala ya vibali.

Nyota hao walibaki huko baada ya kambi kuvunjwa kutokana na sababu ambazo Yanga walieleza kuwa ni kwa maslahi mapana ya klabu.

Wapo wachezaji ambao walitangulia na wanaendelea na mazoezi katika kambi ya Avic iliyopo Kigamboni.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Yanga zimeeleza kuwa wachezaji hao walikuwa wanaendelea na mazoezi hivyo wapo imara.

Ni Yacouba Songne, Dickson Ambundo, Djuma Shaba, Fiston Mayele pamoja na wengine ambao wanatarajiwa kurejea kesho ili kuungana na timu kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi.