Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 19Article 558424

Habari za michezo of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Okwi aibukia Simba Day

Okwi aibukia Simba Day Okwi aibukia Simba Day

Mchezaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ameibukia katika tamasha la Simba (Simba Day).

Okwi alifika uwanjani saa 7:50 mchana akiwa amevalia fulana nyeusi, miwani na jinsi.

Baada ya kufika uwanjani hapo akiwa katika jukwaa la VIP A, mashabiki walilipuka kwa shangwe na kuanza kumshangilia.

Kuna baadhi ya Mashabiki walimvalisha mpaka skafu shingoni kwake ambazo zilikuwa na rangi nyekundu na nyeupe.

Mashabiki wengine wengi wakinguata na kupiga nae picha huku wengine walishindwa kujizuia na kuendelea kumshangilia.

Okwi baada ya kupata mzuka huo mkubwa wa mashabiki wa Simba alikwenda mbele ya eneo la VIP A, na kuanza kuwapungia mkono kwa kuwasalimia.