Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 26Article 539917

Habari za michezo of Wednesday, 26 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

Yanga yaifuata Biashara nusu fainali Kombe la FA

Yanga yaifuata Biashara nusu fainali Kombe la FA Yanga yaifuata Biashara nusu fainali Kombe la FA

Yalikuwa ni makosa ya kizembe ya kipa Mussa Mbissa, yaliyoizawadia Yanga bao dakika ya 25, alipotaka kuleta mbwembwe za kumpiga chenga Kaseke, lakini mchezaji huyo aliunasa mpira na kuujaza wavuni.

Kipa huyo alikuwa amerudishiwa mpira na beki wake, Khalfan Mbarouk, pembeni mwa uwanja na haukuwa na madhara yoyote, lakini alichofanya ni kurudi nao ndani ya 18 na kumsubiri Kaseke ampige chenga, badala yake akaigharimu timu yake bao hilo baada ya kupokonywa mpira na winga huyo.

Kaseke tena, aliwainua vitini wanachama, mashabiki na wapenzi wa timu hiyo, alipoukimbilia mpira mrefu uliopigwa na Yacouba Sogne na kuwazidi mbio mabeki wa Mwadui, kabla ya kuujaza wavuni dakika ya 56.

Kwenye mechi hiyo, Yanga ilitawala hasa katikati mwa uwanja, lakini ilishindwa kutumia nafasi nyingi zilizopatikana kufunga mabao kutoka kwa Feisal Salum aliyekosa mabao mawili ya wazi, Yacouba aliyeshindwa kukwamishwa wavuni akiwa na kipa Mbissa mara tatu.

Nafasi pekee ambayo ilipatikana kwa Mwadui, ilikuwa ni dakika ya 39, baada ya Jabir Aziz kuikosesha timu yake bao, alipopiga shuti juu ya lango la Yanga akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga. Kwa matokeo hayo, Yanga sasa itapambana dhidi ya Biashara United kwenye mechi ya nusu fainali.