Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 26Article 539971

Soccer News of Wednesday, 26 May 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Onyango, Kapombe kuwakosa Dodoma Jiji

Onyango, Kapombe kuwakosa Dodoma Jiji Onyango, Kapombe kuwakosa Dodoma Jiji

Simba itashuka dimba la Mkapa leo saa 1:00 usiku kucheza mechi ya robo fainali dhidi ya Dodoma Jiji katika kombe la (Azam Sports Federation Cup).

Simba wanaingia katika mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kuondolewa katika hatua kama hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs kutoka kwa Madiba.

Katika kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mchezo huo, kocha wa Simba, Didier Gomes amefanya mabadiliko ya wachezaji wawili katika kikosi chake cha kwanza.

Mabadiliko hayo ambayo Gomes ameyafanya ni kupumzisha wachezaji ambao huwa wanacheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza na kuwapa nafasi wengine.

Kulingana na mazoezi ya mwisho wa Simba yaliyofanyika katika Uwanja wa Mo Bunju Arena jana Mei 25, wachezaji waliotolewa katika kikosi cha kwanza ni mabeki, Joash Onyango na Shomari Kapombe.

Nafasi ya Onyango atapewa Kennedy Juma wakati ile ya Kapombe atapewa David Kameta Duchu ambaye alisajiliwa na mabingwa hao watetezi wa kombe hilo msimu huu akitokea Lipuli ya Iringa.   Kulingana na mazoezi hayo kikosi cha Simba kinaweza kuanza hivi; Aishi Manula, Duchu, Mohammed Hussein 'Tshabalala' Keneddy , Pascal Wawa, Taddeo Lwanga, Luis Miquissone, Mzamiru Yassin, Chris Mugalu, Clatous Chama na Rally Bwalya.