Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 22Article 552988

Soccer News of Sunday, 22 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Onyango ni kitasa kweli kweli

Beki wa Simba, Joash Onyango Beki wa Simba, Joash Onyango

Wakati mashabiki wa timu pinzani wakimdhihaki,kumcheka kwa muonekano wake na hata kumuita mzee, hali ni tofauti kwa washambuliaji wanaokutana na beki wa Simba mwenye asili ya kenya Joash Onyango.

Christain Zigah, Straika Mghana anayekipiga Biashara United amesema amekutana na mabeki toauti tofauti Ligi kuu, ila Onyango wa Simba ni zaidi ya beki kwa namna anavyokaba uwanjani.

Zigah amesema alipomuona Onyango kabla ya mechi yao iliyopigwa Februari 18, mjini Musoma alimuona wa rahisi tu, ila shughuli aliokutana nao kwa kisiki hicho Mkenya ulimtoa jasho na timu yao kulala 1-0 kwa bao la mzee wa kuwakera, Bernard Morrison.

“Ukiniuliza ni beki gani mkali niliyekutana naye katika Ligi nitakutajia Onyango, jamaa si wa kusimuliwa, nimekabiliana naye, nilijaribu kutumia mbinu zote, nilishindwa kumzidi ujanja,” amesema Zigah na kuongeza;

“Nilimchukulia pia kwa kuonekana kama ana umri mkubwa, hivyo niliamini asingenidhibiti lakini mambo yakawa tofauti kabisa, huyu jamaa ni zaidi ya beki.”

Onyango hajaitwa katika kikosi cha Harambee Stars kinachojianda na michezo ya kufuzu kombe la Dunia.