Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 586045

Soccer News of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

PSG Hawakati Tamaa Na Mbappe

Kylian Mbappe Kylian Mbappe

Kylian Mbappe amebakiza miezi kadhaa mkataba wake na PSG kutamatika. Vigogo ni wengi milangoni wakisubiri kuiwania saini ya mchezaji huyu.

Ni wakati wa kuamua kubaki au kuondoka PSG kwa Mbappe ambaye, hata sasa, anauwezo wa kusaini mkataba wa awali na timu yeyote nje ya Ligue 1 kama mchezaji huru. Real Madrid wanahusishwa zaidi na Mbappe baada ya kushindwa kumsajili mwaka jana, 2021.

Pamoja na yote yanayoendelea kwenye soko la usajili, Paris Saint Germain wameweka meza ofa mpya ya miaka miwili kwa Kylian Mbappe. Hii ni katika kuonesha kuwa, uongozi wa klabu hiyo bado unamuhitaji mchezaji huyo na, hawajakata tamaa na harakati za kumbakiza klabuni hapo.

Hata hivyo, Mbappe ameamua kuachana na habari za usajili wakati huu ambao anaelekeza nguvu na mawazo yake kwenye kumaliza msimu na kisha, ataamua hatma yake baada ya msimu huu kutamatika.